MSANII MAARUFU NCHINI KENYA JAGUAR AWASILI TANZANIA,TAYARI KWA KUANGUSHA BONGE LA SHOO KWENYE TAMASHA LA BODA KWA BODA BEACH CONCERT - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MSANII MAARUFU NCHINI KENYA JAGUAR AWASILI TANZANIA,TAYARI KWA KUANGUSHA BONGE LA SHOO KWENYE TAMASHA LA BODA KWA BODA BEACH CONCERT

Mwanamuziki mahiri nchini Kenya ajulikanae kwa jina la JAGUAR,awasili nchini Tanzania tayari kwa kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la BODA KWA BODA BEACH CONCERT.

Kuzungumzia na uthibitisho wa ujio wa Mwanamuziki huyo Dar,Meneja wa Masoko wa kampuni ya G5 CLICK COMPANY,Desy Ernest amesema kuwa,Mwanamuziki Jaguar kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la BODA KWA BODA BEACH CONCERT litalojiri pande za Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar Es Salaam mnamo November 12 (LEO) majira ya saa moja jioni.Akisindikizwa jukwani na wasanii wakibongo wakiwemo Sumalee,GodZilla,Country Boy & Stamina,Young D,Beka na wengineo wengi tu
Desy Ernest amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za BODA KWA BODA BEACH CONCERT zitakuwa tofauti na wenye msisimko mkubwa, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani ya Tanzania. Jaguar awasii mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ilikukamilisha mpango mzima  wa BODA KWA BODA BEACH CONCERT.





Picha Zote Na G5 Click

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages