Mratibu
wa mradi wa MWEI wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw.
Mgongo Emmanueley akitoa mafunzo ya awali kwa wanawake wa Usagara Mkoani
Mwanza kuhusiana na mradi huo utakaowapa fursa mbalimbali za kujikwamua
kiuchumi katika biashara zao ndogondogo.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakipata maelekezo ya kutumia huduma
ya M-pesa kutoka kwa Mratibu wa mradi huo Bw. Mgongo Emmanueley wakati
mafunzo hayo yenye kuwawezesha kujikwamua kiuchumi yakiendelea huko
Usagara Mkoa wa Mwanza.
Kikundi
cha wanawake kutoka Usagara Mkoani Mwanza wakipata maelekezo ya namna
ya kutumia huduma ya M-pesa katika simu zao za mkononi kutoka kwa
Mratibu wa mradi wa MWEI Bw. Mbuyu Ally unaoendeshwa na kampuni ya simu
za mkononi ya Vodacom Tanzania ukiwa na lengo la kuwawezesha wanawake
kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao ndogondogo.
Mratibu
wa mradi wa MWEI unaoendeshwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania Bw. Mgongo Emmanueley (wan ne kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na kikundi cha wanawake wa Usagara Mkoa wa Mwanza mara baada ya
kumalizika kwa mafunzo kuhusu mradi huo ambao pia utawawezesha
kujikwamua kiuchumi kupitia biashara zao ndogondogo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)