Miss
Tanzania 2011, Salha Israel amefanikiwa kuingia nusu fainali ya taji la
Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) yaliyofanyika juzi
nchini Uingereza.
Akizungumza
kutoka London jana, Salha alisema kuwa katika taji hilo, mrembo huyo
aliwasilisha kazi yake ya Jamii aliyoifanya kwenye hospitali ya
Muhimbili ambako alisaidia watoto wenye matatizo ambao wanazaliwa chini
ya mwezi moja.
Salha
alisema kuwa katika shindano hilo, Salha aliwakilisha DVD inayonyesha
jinsi gani alivyomsaidia mtoto aliyezaliwa kwenye hospitali hiyo huku
akiwa na kidonda kikubwa mgongoni.
“Haikuwa
kazi rahisi kwa majaji wa shindano hilo kuona ninavyofanya kazi ya
kumsaidia mtoto huyo, ni kazi ambayo imewafanya waikubali kwani ipo
katika majukumu ya Kamati ya Miss World mbali ya shindano lenyewe la
urembo,” alisema Salha kwa njia ya simu.
Alisema
kuwa amefarijika kuingia katika hatua hiyo ya 16 bora katika shindano
hilo ambalo lilishirikisha jumla ya warembo 122 kutoka nchi mbali
mbali.
“Ninachokisubiri sasa ni fainali ya taji hili ambapo mshindi ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo itashirikisha si chini ya warembo 20,” alisema.
Kuhusiana
na mashindano, Salha alisema kuwa mashindano ni magumu ukilinganisha na
mashindano ya Miss Tanzania kutokana na mambo makubwa moja.
Alisema
kuwa sababu hiyo ni idadi ya washiriki ambao ni wengi ukilinganisha na
warembo 30 wanaoshiriki Miss Tanzania na vile vile wapo bora zaidi
kulinganisha na mashindano ya kitaifa.
“Ninawaomba Watanzania ni waniombee ili niweze kufanya vyema katika mashindano, ni magumu kwa kweli,” alisema.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Hashim "Uncle" Lundenga alimpongeza Salha
kwa hatua hiyo na kusema japo anakabiliwa na kibarua kikubwa ili aweze
kufanya vyema.
"Ni matokeo mazuri, lakini kazi bado ni kubwa, tunatakiwa kumwombea ili aweze
kufanya vyema zaidi," alisema Lundenga.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)