MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AZINDUA KAMPENI YA CHANJO YA UGONJWA WA SURUA NA POLIO KWA WATOTO, KITAIFA JIJINI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AZINDUA KAMPENI YA CHANJO YA UGONJWA WA SURUA NA POLIO KWA WATOTO, KITAIFA JIJINI ARUSHA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpa tone la dawa ya Chanjo mtoto, Renatha Faustine (1) wakati wa alipokuwa akizindua Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011. Aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto huyo, Selina Hando Mkazi wa Moshono Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011.
Watoto wa Shule za Msingi, wakipita mblele ya jukwaa la mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya  Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages