Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.
Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa
na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya
kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni
mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa
alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka
1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
Juu ya kutolewa kwake,
Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza
wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki
zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)