Jiji la dar na zanzibar visiwani kukosa umeme kwa siku kadhaa kufuatia kulipuka kwa transifoma ubungo jioni ya jana. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Jiji la dar na zanzibar visiwani kukosa umeme kwa siku kadhaa kufuatia kulipuka kwa transifoma ubungo jioni ya jana.

Moja ya Transifoma iliyopo katika Kituo cha Umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam (Ubungo Grid Sub Station) imeungua moto jioni ya jana. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Naibu Mkurugenzi wa Tanesco, Bi. Sophia Mgonja amesema kuwa, kutokana na hitilafu hiyo Jiji la Dar es Salaam na Visiwa vya Zanzibar vitakosa umeme kwa siku kadhaa. Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo, Mgonja alisema lilitokea baada ya kifaa cha kurekebisha nguvu ya umeme kiitwacho Reactor kuungua. Picha hizi zinawanyonyesha wafanyakazi wa kikosi cha zima moto wakizima moto katika Transifoma iliyokuwa ikiungua.
Picha kwa hisani ya Kulwa Mwaibale/Global Publishers .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages