HATIMAYE
kitendawili cha nani ataibuka Malkia wa Dunia 2011, kimeteguliwa kwa
Miss Venezuela2011, Ivian Sarcos usiku wa Jumapili Novemba 6, 2011
kufanikiwa kutawazwa kuwa Malkia Mpya wa Taji la Urembo la dunia “Miss
World 2011, hulku matumaini ya Tanzania kupitia kwa Miss Tanzania 2011,
Salha Izrael Kifai yakigonga mwamba kwa mara nyingine tena katika
mashindano hayo.
Katika
shindano hilo la aina yake lililofanyika katika ukumbi wa Earls Court
in London, Sarcos mwenye umri wa miaka 21 alifanikiwa kuwatupa nje zaidi
ya warembo 100 kutoka nchi mbalimbali Duniani katika shindano hilo
ambalo lilikuwa ni la 61 tangu kuanzishwa kwake.
Nafasi
ya pili ilikwenda kwa Miss Philippines 2011, Gwendoline Ruais na nafasi
ya tatu ikienda kwa Miss Puerto Rico 2011, Amanda Perez.
Bara
la Afrika lilifanikiwa kuingiza warembo wawili katika hatua ya makundi
ya 15 bora ambapo mrembo kutoka nchini Zimbabwe na jirani zao Afrika
Kusini ndio waliolitoa kimasomaso bara hilo.
Afrika
tena ikabahatika kuingia katika hatua ya 7 bora ya Miss World pale
mrembo kutoka Afrika Kusini alipofanikiwa kuingia katika hatua hiyo.
Shindano
hilo lilianza kufanyika saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
lilipambwa na burudani mbalimbali za muziki kutoka kundi la Vijana wa
Uingereza la street dance troupe Diversity, wakifuatiwa na utambulisho
wa Washiriki wote wa Miss World 2011.
Shindano hilo lilifikia tamati pale Miss World 2010 Alexandria Mills alipopanda jukwaani na kumvika taji Sarcos.Kwa Hisani Ya Uniquee Entertainment
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)