Godbless Lema aachiliwa huru mpaka Disembe 14 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Godbless Lema aachiliwa huru mpaka Disembe 14

Na Gladness Mushi Arusha
Mbunge wa jimbo la arusha mjini Bw. Goodbless Lema leo ameachiliwa huru na mahakama ya hakimu mkazi mara baada ya kukidhi vigezo vya mahakama katika kesi ambayo inamkabili mbunge huyo ya kufanya maandamano na mkusanyiko bila kibali maalumu cha vyombo vya usalama. Hayo yalikuja mara baada kudaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa namba moja ambaye ni Mbunge wa jimbo la arusha mjini kuwa nje kwa dhamana hadi Disemba 14 mwaka huu Aidha hakimu ambaye anasikiliza kesi hiyo Bi Judith Kamala aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo kisheria yupo huru kwa kuwa vigezo vya mahakama vilidai kuwa mtuhumiwa huyo namba moja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili jambo ambalo walikidhi vigezo hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa ambapo itasikilizwa tena mahakamani hapo Disemba 14 mwaka huu. Katika hatua nyingine mbunge huyo aliambia vyombo vya habari kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo anatakiwa kuacha ushabiki wa kisiasa na kama hataweza kuacha ushabiki huo atalazimika kuwatumia wanawake yaani mke wa mbunge na mke wa mkuu wa mkoa ili waweze kusuluishana. Aidha Bw. Lema alisema kuwa hatua hiyo itakuja kwa kuwa mara nyingi mkuu huyo ameonekana akisema na kuwatetea chama cha mapinduzi hali ambayo inachangia unyanyasaji mkubwa sana Aliongeza kuwa hali hiyo ya kumtuma mke wake kwenda kwa RC mkoa wa Arusha huenda ikaleta maafanikio zaidi kwa kuwa wanawake kwa wanawake wanaweza kusikilizana tofauti na wao ambao mpaka sasa tofauti zimeshajitokeza sana. katika hatua nyingine Bw Lema aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kujua na kutambau kuwa yeye si mwehu kukataa dhamana na badala yake wanatakiwa kujua kuwa anatafuta haki ambayo inaondolewa na baadhi ya vyama vya siasa pamoja na Jeshi la polisi Alibainisha kuwa kwa kuwepo kwake Gerezani ameweza kugundua na kujua kuwa ndani ya jeshi la polisi wapo baadhi ya askari ambao wanakiuka taratibu za jeshi hilo na kuwapa watu kesi ambazo si za kwao hali ambayo inasabbaisha madhara makubwa sana kwa wananchi hasa wale wenye kipato cha chinil. Bw Lema alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wana kemea vibaya tabia ya kunyimwa haki zao za msingi na pia wananchi hao wana haki

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages