MTUNISHA
misuli maarufu wa Tanzania, David Nyombo anaondoka (kesho jumatano)
kwenda Mumbai, India kushindana katika taji la dunia la Mr. Universe.
Nyombo
ambaye mwaka jana alimaliza nafasi ya nne katika mashindano ya Anold
Classic nchini Marekani, amesema kuwa amejiandaa vilivyo tayari kurejea
na ushindi hapa nyumbani. Alisema kuwa mashindano hayo yanayofanyika kuanza Novemba 3 mpaka 7, yatashirikisha zaidi ya watunisha misuli 180 kutoka nchi mbali mbali Duniani.
“Nimejiandaa
vilivyo kwa ajili ya mashindano haya, nimetumia fedha zangu mwenyewe na
msaada kutoka kwa marafiki zangu, lengo langu kubwa ni kuitangaza nchi
nje ya mipaka na si vinginevyo,” alisema Nyombo. Alisema
kuwa pamoja na wadhamini wengi kushindwa kumsaidia, anashukuru juhudi
zake zimefanikiwa na sasa anakwenda kuipeperusha bendera ya Tanzania
nje ya mipaka.
“Ningeweza
kusema sina fedha, watu wangenielewa japo nusu nusu, lakini nikaona
kuwa fedha si kikwazo kwangu, najua watu watanipongeza mara
nitakapofanya vizuri kama ilivyokuwa katika mashindano ya nyuma,”
alisema Nyombo ambaye mwaka 2009 alishinda taji la Mr. Afrika.
Alisema kuwa anajua kuna ushindani, lakini yeye amejidhatiti zaidi katika uzani wa welter na bila shaka anaibuka kidedea. Alisema
kuwa katika mashindano ya mwaka jana nchini Baku, alibuka dani ya 12
bora, na katika mashindano yaliyofuata, alifanya vizuri zaidi na hicho
ndicho kigezo cha kumwezesha kufanya vyema.
Mbali
ya kushindana, Nyombo pia ataiwakilisha nchi katika mkutano wa mwaka wa
Shirikisho la Mchezo huo Duniani, IFBB akiwa kama mjumbe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)