AJALI YA BASI YAUA MMOJA, YAJERUHI 20 MOROGORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AJALI YA BASI YAUA MMOJA, YAJERUHI 20 MOROGORO

Hali ilivyokuwa katika eneo la ajali.
MTU mmoja amekufa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya basi la Master City lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, kupinduka eneo la Makunganya mkoani Morogoro leo asubuhi.

Aliyefariki ni Salum Amir (47) aliyekuwa utingo wa basi hilo ambaye ni mkazi wa Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.  Majeruhi ambao hali zao si mbaya sana wamepatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro, Leonard  Gido, alisema chanzo cha ajali ni mwendo wa kasi.

Picha zaidi za tukio hilo:


PICHA HABARI NA DUNSTNA SHEKIDELE/GPL,MOROGORO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages