AJALI YA BASI LA SUMRY NA PRADO MKOANI IRINGA JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AJALI YA BASI LA SUMRY NA PRADO MKOANI IRINGA JANA

Baadhi ya abiria wakimwangalia dereva wa Prado aliyefariki papo hapo baada ya ajali hiyo.
Basi la Sumry likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo.
Majeruhi katika ajali hiyo wakijinasua kutoka kwenye basi la Sumry.
PICHA mbalimbali za ajali mbaya iliyotokea jana katika sehemu ya Mtandika, mbele kidogo ya hoteli maarufu ya Al Jazeera, mkoani Iringa, iliyohusisha basi la Sumry na gari aina ya Prado iliyokuwa ikiendeshwa na daktari bingwa wa macho katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Katika ajali hiyo daktari huyo alifariki papo hapo (kama inayoonekana katika picha), Na katika basi hakuna aliyepoteza maisha licha ya majeraha madogo madogo. Dereva wa basi alikimbia baada ya ajali hiyo na hivi sasa anatafutwa na jeshi la polisi.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita lori (ku-overtake) katika kona na kukutana uso kwa uso na gari hiyo aina ya Prado ambayo pia ilikuwa katika kasi.


Picha zote na: www.latestnewstz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages