Walioteketea kwa moto
inadhaniwa kuwa ni dereva na tandiboy waFuso ambao walibanwa katika gari
hilo baada ya kukatika cabin.
Fuso ilivyoteketea kabisa na
moto.
Watu zaidi ya wawili
wanahofiwa kufa katika ajali ya gari iliyotokea usiku majira ya saa 6
katika eneo la kijiji cha Mdori Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo
watu wawili walionekana miili yao ikiwa imeungua na moto. Ajali hiyo
ililihusisha roli la mizigo lililokuwa limetokea Arusha na Fuso
lililokuwa limetokea Singida.
Mafuta ya kupikia ya
alizeti yalitapakaa katika eneo hilo.
Wanawake wa Kijiji cha Kadori wakichota
mafuta yaliyomwagika katika ajali hiyo.Lakini je mafuta haya
yaliyomwagika chini ni safi na salama kwa afya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)