Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru alipokwenda kuzindua rasmi kadi ya Debit Master Card ya NBC jijini Dar es Salaam Jumanne jioni. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Mwinda Kiula-Mfugale.
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) na Mwakilishi wa Master Card katika nchi za Afrika Mashariki na Visiwa vya Bahari ya Hindi, Chariton Goredema wakionyesha mfano wa kadi ya Debit Master Card ya NBC katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi hiyo jijini Dar es Salaam Jumanne jioni.
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) alipokwenda kuzindua rasmi kadi ya Debit Master Card ya NBC jijini Dar
es Salaam Jumanne jioni. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk Mussa Juma Assad.
es Salaam Jumanne jioni. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk Mussa Juma Assad.
Mkuu wa Kitengo cha Shughuli za Kibenki wa NBC, William Kallaghe akimpokea Waziri wa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kabla hajazindua rasmi kadi ya Debit Master Card ya benki hiyo jijini Dar es Salaam Jumanne jioni. Kulia ni Mkuu Rasilimali Watu wa NBC, Blasius Lupenza.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki hiyo, Maharage Chande huku Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale akisikiliza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya Debit Master Card ya NBC Jumanne jioni jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari akijadili jambo na Mshauri wa Mambo ya Habari wa benki hiyo baada ya uzinduzi wa NBC Debit Master Card jijini Dar es Salaam juzi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)