Kikundi
cha Sanaa cha Jambo brothers kutoka Zanzibar kikionyesha sarakasi
mbalimbali katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi (latham
Open) yaliyokuwa yakiendelea kisiwani humo, ambayo pia yalidhaminiwa
na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Commodore
Spiras Manoloudis wa Yatch Club jijni Dar es Salaam (kushoto) akitoa
neon la shukrani kwa wadhamini wa mashindano ya uvuvi (latham Open)
yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda hivi karibuni ambao ni Kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, (kulia) Mkuu wa Udhamini wa Vodacom
Bw. George Rwehumbiza.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia)
akimkabidhi zawadi Alfred Charles kwa niaba ya timu yake baada ya
kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa boti ya Mistress katika
mashindano yaliyofanyika huko Sinda kisiwani mwishoni mwa wiki na
kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Washindi
wa mashindano ya uvuvi ya Latham Open wakifurahia tuzo zao za ushindi
mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika
Kisiwani Sinda mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mwanamuziki
Mark Hart kutoka Afrika Kusini akitumbuiza katika mashindano ya uvuvi
yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, mashindano hayo
yaliyoshirikisha nchi sita yalidhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi
ya Vodacom Tanzania.
Wafanyakazi
wa boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki zilizovuliwa katika kisiwa
cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi yajulikanayo kama Latham Open
yaliyoshirikisha nchi sita na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi
ya Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)