Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua BaloziJuma Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo Kikuu cha Dodoma kuanziatarehe 14 Septemba 2011.Atakuwa
kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne (4)
Balozi Mwapachu anachukua nafasi i liyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kwanza na sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.
Mhe. BaloziJuma Mwapachu amewahi kushi ka nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo Katibu Mkuu wa Jumu iya ya Afrika Mashariki, Baloziwa Tanzania nchini Ufaransa ikijumuishanchiz a Uhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria. AidhaMhe. BaloziJuma Mwapachu amekuwa mjumb e wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahi kushika nyadhifa za juu kati kaTaasisiza Umma na binafsi. Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenye kitiwabaraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mhe. BaloziJuma Mwapachu amehitimu sha hada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanza niawa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunga naJeshi la Polisi nchini.
Mhe. BaloziJuma Mwapachu aliwahi kutun ukiwa shahada ya heshima ya udaktar i wafalsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.
Uongozi wa Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu cha Dodoma inamkaribisha na kumtakia kila la kheri BaloziJuma Mwapachu katika m ajukumu yake mapya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)