usalama wa taifa na vita dhidi ya wapiga picha Tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

usalama wa taifa na vita dhidi ya wapiga picha Tanzania


Maofisa wa usalama wa Taifa wakiwa wamemnyang'anya kamera na kumtoa eneo lake la kazi Mpigapicha wa magazeti ya The Guardian na Nipashe, Khalfan Said wakati wa ujio wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo. 
Maofisa hao wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wapigapicha za habari kufaya kazi zao kwa uhuru jambo linalosababisha kero kwa wapigapicha nchini na hata wakati mwingine kufikia kuwanyang'anya vitendea kazi vyao, kupigwa. Vitendo kama hivi pia vimekuwa vikifanywa na Polisi jambo ambalo linaleta taswira kuwa Wapigapicha nchini ndio watu hatari zaidi kwa vyombo hivi viwili vya usalama.Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages