Katibu
wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (aliyesimama) akitoa taarifa kwa wageni
wanaoshughulikia mambo ya afya kutoka Marekani pamoja na uongozi wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini 0kt-20-2011 katika Ofisi za
WAMA walipokutana na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama
Salma Kikwete kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu kusaidia kuleta
vifaa tiba kwaajili ya jitihada za kupunguza vifo vya akina mama na
watoto wachanga nchini.
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Zakhia Meghji (kulia) akibadilishana
mawazo katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam Oktoba 20,2011 na
wajumbe kutoka Marekani wa taasisi inayotambulika kama GE
healthymagination inayoshughulikia mambo ya huduma za afya ( kushoto) ni
Mkurugezi wa Global Programs healthymogination Joneen UzzelI na
(aliesimama katikati) ni Mkurugenzi mwenza wa mpango wa ushirikiano wa
wake wa Marais wa nchi za Afrika (( Co- Director of African First Ladies
Fellowship Program) Cora Neumann, wakati ujumbe huo ulipokwenda
kumtembelea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
(hayupo pichani ) na kuzungumzia jinsi ya kusaidia kuleta vifaa tiba kwa
ajili ya kusaidia kupunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga
nchini .
Katibu
wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (kulia) akiagana na Mjumbe kutoka
Marekani wa Taasisi hiyo(kushoto) Reza Bundy baada ya kumaliza
mazumgumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, (pichani
hayupo) Mazungumzo hayo pia yamewahusisha wataalamu kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa jamii wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Blandina Nyoni hayupo pichani – Oktoba 20-2011.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)