Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Lawrence Mafuru (kulia)
wakibadilishana hati za makubaliano kuhusu suala la mikopo ya nyumba
jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu akisaini hati
za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Lawrence Mafuru
kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia
ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka
na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (kushoto)
akishikana mikono na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence
Mafuru katika hafla ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilisaini
hati za makubaliano kuhusu mikopo ya nyumba na benki saba nchini. Benki
hizo ni NBC, NMB, BOA, EXIM, Azania, KCB na CBA. Wa pili kushoto ni
Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT) Lila Mkila na Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (katikati,
nguo nyekundu), Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu (wa nne kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki saba zilizosaini
makubaliano ya ushirikiano na NHC.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)