Takriban watu 55 wameuawa na kinachodhaniwa kuwa
mlipuko mkubwa uliofanywa na mtu aliyejitoa mhanga karibu na jengo la
serikali kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Walioshuhudia wamesema lori lililokuwa na
milipuko lilikwenda moja kwa moja kwenye lango karibu na wizara moja ya
serikali na kulipua.
Sheikh
Ali Mohamed Rage, msemaji wa kundi la wanamgambo la al-Shabab,
aliiambia BBC kuwa wamehusika kwenye shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC wa Somalia Mohammed Dore
alisema magari yalikuwa yamechomwa moto, miili ilionekana ikiwa imezagaa
mitaani na askari waliopata mshtuko walikuwa wakifyatua risasi ovyo. Mwandishi wetu alisema, miongoni mwa waliouawa
na kujeruhiwa ni wanafunzi waliokuwa wamepanga foleni katika lango kuu
kufanya mtihani katika wizara ya elimu ili kupata ufadhili wa kusoma
Uturuki.
Alisema ni tukio baya zaidi yeye binafsi
kushuhudia.
Viongozi wa serikali ya mipto inayodhaminiwa na
umoja wa mataifa walikuwa wakikutana kwenye jengo hilo wakati shambulio
hilo lilipotokea. Hata hivyo, bado haiko wazi iwapo ni miongoni
mwa waliofariki dunia.
Afisa mmoja kutoka Umoja wa Afrika, yenye
majeshi yake ya kutunza amani Somalia, alisema tukio hilo "ni la hatari
sana".
Source: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)