Serikali ya China yatoa msaada wa mipira 300 kwa serikali ya tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Serikali ya China yatoa msaada wa mipira 300 kwa serikali ya tanzania

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.) akipewa maelezo na Balozi wa China nchini, Bw. Liu Xinsheng (aliyeinama) kuhusu Baiskeli zilizotolewa kwake na Ubalozi huo. Ubalozi huo pia umemkabidhi Waziri mipira 300 kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu. Aidha, Ubalozi wa China umetoa vifaa vya michezo ya Kichina kwa Chama cha Wushu Tanzania. Vifaa hivyo vimetolewa leo katika Ubalozi wa China

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.) na Balozi wa China nchini, Bw. Liu Xinsheng, wakipeana hati za makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini leo katika Ubalozi huo. (Picha na Concilia Niyibitanga- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages