Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa
Mama wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Professa Beno Ndulu kufuatia
kifo cha mama yake mzazi Bibi.Regina Steven Mpangile kilichotokea
juzi(30/9/2011) katika hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es
Salaam.Kushoto aliyesimama ni Professa Beno Ndulu.Marehemu Regina
anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kinondoni. Rais Kikwete
alikwenda nyumbani kwa marehemu ,Tabata jijini Dar es Salaam kutoa pole
na kuifariji familia ya marehemu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu Professa
Beno Ndulu wakiwafariji ndugu na jamaa wa mama wa Gavana Marehemu
Bibi.Regina Steven Mpangile nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es
Salaam leo jioni.Maremu Bibi Regina alifariki juzi katika Hospitali ya
Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa
kesho(jumatatu) katika makaburi ya Kinondoni. Picha na Freddy Maro wa Ikulu







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)