Msanii Mahiri Kutoka nchini Angola Cabo Snoop Atua Jijini Dar es Salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Msanii Mahiri Kutoka nchini Angola Cabo Snoop Atua Jijini Dar es Salaam

Msanii mahiri kutoka nchini Angola,ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake kadhaa hapa nchini,ikiwemo wimbo wa Prakatatumba na Windeck,baada ya kulitikisha jiji la Nairobi kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011 lililofanyika jana,jioni ya leo ametua jijini Dar kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere akiwa ameambatana na Crew yake,msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza Oktoba 9, ambayo itakuwa  ni siku ya kifamilia a.k.a Family Day kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Pichani mlangoni shoto ni Cabo Snoop akiwa ameambatana na mwenyeji wake kutoka Kampuni ya Prime Time Promotion,Balozi
Kindamba,mbele kabisa ni Meneja wa msanii huyo
Pichani kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga akitoa maelekezo mafupi,mara baada ya kuwasili kwa msanii huyo Cabo Snoop na Crew yake jioni ya leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa Jk Nyerere,jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages