Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw.
Michael Shirima (kulia) akitoa tamko rasmi kuhusiana na mpango wa Uuzaji wa Hisa katika
Soko la Awali (IPO) utakaoanza tarehe 7 Oktoba mpaka tarehe 28 mwezi huu. Tamko
hilo lilitolewa na Mwenyekiti huyo mapema leo katika Hoteli ya ‘Kilimanjaro’
Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko
akifuatiwa na Meneja Uhusiano wa Wateja katika Benki ya Stanbic Bi. Naomi
Vincent.
.....................................................

TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Dar es Salaam Oktoba 4, 2011. Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la
ndege la Precision Air Services Plc inapenda kuwataarifu kwamba mpango wetu wa
Uuzaji wa Hisa katika Soko la Awali (IPO) na kuorodheshwa katika Soko la Hisa
la Dar es salaam (DSE) imepatiwa vibali vyote husika na sasa ipo tayari kwa
hatua zinazofuata.
Kilichoidhinishwa
ni ratiba ya matukio ya utaratibu mzima wa mchakato huu:
Tarehe ya Ufunguzi wa Ofa
|
Oktoba 7
2011 ; 0300 asubuhi
|
Tarehe ya Kufungwa kwa Ofa
|
Oktoba 28 2011 ; 1000 jioni
|
Kutangazwa kwa matokeo ya Ofa
|
Novemba 11 2011
|
Kuingiza hisa katika akaunti za CDS, kutoa risiti/cheti za malipo na
marejesho ya hundi
|
Novemba 25 2011
|
Kuorodheshwa na kuanza biashara ya kununua na kuuza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
|
Desemba 8 2011
|
Kampuni
itatoa jumla ya hisa 58,841,750 kwa ajili ya ununuzi kwa bei ya 475 kwa kila hisa.
Huku idadi ya chini ya kuanza kununua hisa ambayo mtu ataruhusiwa kununua
itakuwa ni hisa 200.
Nakala
ya waraka wa matarajio ya kampuni ambayo pamoja na mambo mengine, maelezo
maalumu ya ufafanuzi na ununuzi wa hisa zinapatikana katika tovuti ya Precision
Air www.precisionairtz.com tarehe 4
Oktoba 2011.
Kwa
niaba ya Wakurugenzi ya Bodi, utawala na wafanyakazi wote napenda kutoa
shukurani zangu za dhati kwa wateja wetu kwa mchango wao na ushirikiano
yakinifu ulioweza kufanikisha maendeleo na ukuaji wa shirika la ndege hili
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.
...…………………………….
Michael N Shirima
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)