Shirika hilo lilitembelea magereza 20 na
kusema kuwa limepokea ripoti kuwa wafungwa sita waliteswa katika vituo
vinavyosimamiwa na wanajeshi watiifu kwa Baraza la Mpito NTC.
Walinzi katika vituo hivyo wanatuhumiwa
kuwadhulumu wafungwa katika magereza hayo ya muda kwa kuwapiga viboko na
hata kuwatesa kwa kutumia umeme.
Aidha Shirika hilo linasema wafungwa
wanaotuhumiwa kuhusika na visa vya ubakaji na mauaji walionekana
kudhulumiwa zaidi na kushurutishwa kukiri mashtaka dhidi yao na walinzi
katika magereza hayo.
Shirika hilo la 'Human rights watch',
limetoa wito kwa Baraza hilo la Mpito, kubuni mfumo wa haki ambao
utahakikisha kuwa wafungwa wote wanapewa haki sawa za kibinadamu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)