NBC yaipiga jeki Sekondari ya Wasichana Ilulu-Kilwa Yatoa msaada wa vifaa vya maabara. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NBC yaipiga jeki Sekondari ya Wasichana Ilulu-Kilwa Yatoa msaada wa vifaa vya maabara.

Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya maabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Ilulu, Wilaya ya Kilwa. Mkoani Lindi jana. Vifaa hivyo vina thamani ya shs milioni tano. Kushoto ni Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa huo na mlezi wa sekondari hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila (wa pili kushoto) akiwa na  Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kushoto kwake) katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya maabara kwa  ajili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Ilulu, Wilaya ya Kilwa, mkoani humo jana. Vifaa hivyo vina thamani ya shs milioni tano. Kushoto kabisa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa huo na mlezi wa sekondari hiyo na kushoto kwa Masanja  ni Meneja wa NBC Lindi, Godfrey Chilewa.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ilulu, Said Meck Sadik ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vya maabara kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Godfrey Chilewa (kushoto), vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya sekondari hiyo shuleni hapo Kilwa Mkoani Lindi jana. Vifaa hivyo vina thamani ya shs milioni tano. Kulia ni Mkuu wa sasa wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages