Mtoto Sesilia Edward,alipowasiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa New Delhi Nchini india
Mtoto Sesilia Edward,akiwa hospitali ya Fortis iliyopo New Delhi, tarehe 27 septemba mwaka huu
Mtoto Sesilia Edward akiwa wodini nchini india
Mtoto Mwenye ugonjwa unaofanana na Mtoto Sesilia ambae alilazwa wodi moja nae nchini india
----
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 18 Oktoba 2011
Mtoto
Sesilia Edward, mwenye umri wa miaka 14 ambaye alisafirishwa kwenda
nchini India, katika hospitali ya Fortis iliyopo New Delhi, tarehe 27
septemba mwaka huu, kwa ajili ya matibabu ya moyo, amewasili salama
nchini.
Baada
ya kupokelewa alipofika nchini India, Sesilia alianza kufanyiwa
uchunguzi wa kina na kujulikana kuwa chemba ya juu ya kulia ya moyo
wake, imekuwa kubwa kupita kawaida, huku chemba ya chini ya kulia ikiwa
ni ndogo kupita inavyotakiwa kuwa, jambo lililopelekea uvujaji katika
valvu iitwayo Tricuspid pamoja na kuonekana kwa kimiminika (maji maji)
katika tumbo pamoja na mapafu.
Tatizo kama hili lililomkumba Sesilia, liitwalo kwa jina la kitaalamu kama Endomyocardical Fibrosis,
hutokea mara chache. Taarifa za madaktari nchini India, zinaeleza kuwa
hatua ya kiafya aliyofikia Sesilia katika tatizo hili ni mbaya, hivyo
imepelekea kushindwa kutibika kwa ugonjwa huu hivyo atahitaji uangalizi
mkubwa kwa kutumia dawa na sio kwa upasuaji wowote ule wa moyo.
Kwa
dawa ambazo Sesilia ameanza kutumia mpaka sasa, ameweza kupungua kwa
kilogramu tano, anajisikia nafuu zaidi, na afya yake inaimarika. Ugonjwa
kama wa Sesilia umesharipotiwa kutokea kwa watoto katika maeneo ya
Zanzibar, Pemba, kisarawe Tanzania na Kerala- kusini mwa India. Dokta
Srah Matemu kutoka Hospitali ya Regency amesema kuwa watoto zaidi ya
asilimia 20% wanaofanyiwa upasuaji katika hali kama ya Sesilia huwa
hawaponi na hivyo madaktari wa hopitali ya Fortis waliamua kutomfanyia
operesheni hiyo.
Aidha, tatizo hili limehusishwa na ulaji uliopitiliza wa mihogo yenye sumu iitwayo Cyanide
inayopelekea kuvuja na mishipa kusikotakiwa na kudhoofu katika mishipa
ya moyo. Katika miaka mitano iliyopita,Sesilia alikuwa akitumia mlo wa
muhogo mara tatu kwa siku, amekiri katika kipindi hicho chote, ni mara
chache sana amekuwa akila vyakula vingine kama uji,ugali,au wali .
(Sesilia ni mzaliwa wa Kisarawe na amesihi kijijini hapo kwa miaka
takribani 13).
Sesilia
ataendelea na matibabu na uangalizi zaidi katika hospitali aliyokuwa
akitibiwa awali, hospitali ya taifa Muhimbili, huku hospitali ya Regency
ikijitolea kumsaidia matibabu ya kupunguza maji na dawa mbalimbali kwa
garama nafuu..
Ili
kuepuka kutokea kwa tatizo kama hili kwa watoto wengine, Wazazi
wanashauriwa kuwa waangalifu katika kupanga milo ya watoto.Uzidishaji
wa chakula cha aina moja unaweza kuleta madhara kwa afya ya mtoto kama
madhara ya mihogo. Pia kipindi wanapoona watoto wao hawako sawa kiafya,
wawahi hospitali kwa ajili ya matibabu ili kuepuka kukomaa kwa tatizo
kunakoweza kupelekea ugonjwa kutotibika. (Dr. Sarah Matemu)
Kipindi
cha Mimi na Tanzania, kinatanguliza shukrani zake za dhati kwa timu
nzima ya Africa Media Group, iliyoshiriki kwa kiasi kikubwa katika
kufanikisha zoezi la uhamasishaji wa uchangiaji wa pesa kwa ajili ya
safari na matibabu ya Sesilia ambayo yamefanyika nchini India.
Pia
shukrani ziifikie hospitali ya Fortis Escorts Heart Institute, ambao
ilijitolea kwa kupunguza bei ya matibabu ya Sesilia, bila ya kuisahau
hospitali ya Regency Dar es Salaam, chini ya uongozi wa Dk. Kanabar kwa
kumuandaa Sesilia kimatibabu kwa mda wa wiki moja kabla ya kumsafirisha
India kwa ikiwa ni pamoja na daktari kutoka nchini aliyewasindikiza,
aitwaye Dk. Ali Amour kutoka hospitali ya Mnazi mmoja.
Shukrani
pia zinatangulizwa kwa uongozi mzima wa Lions Club, kwa kufanikisha kwa
kuandaa mipango ya matibabu yote ya Sesilia na hospitali, nchini India
ambayo yalifanyika kwa bei ya chini kuliko ambavyo hata raia wa India
angeweza kutibiwa.
Zaidi
ya yote, Mimi na Tanzania inapenda kuwashukuru kwa hali na mali
watanzania wote walioguswa na mtoto Sesilia, na kujitokeza kwa kumsaidia
kifedha, mavazi na hata kwa sala ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine
yoyote binti huyu aliyokuwa akihitaji.Moyo wa upendo na huruma
mlioonyesha kwa mtoto huyu ni zawadi isiyosahaulika katika maisha yake
na wanaomzunguka. Tusiache kuwasaidia na kubadilisha maisha ya ndugu
zetu wahitaji kama hawa. Shukrani!
Usiache
kutizam kipindi cam Mimi na Tanzania Jumapili tarehe 22 Oktoba, saa
1:30 jioni – Chanel Ten, kumsikia Dokta Sarah akielezea nini Hatima ya
Mtoto Sesilia.
Vyomba
vya Habari Tanzania, tumejaribu, tumeweza na yaliyotokea kwa mtoto
Sesilia ni kazi ya Mungu. Fedha zilizobaki zitahifadhiwa katika account
ya Mlezi wake chini ya uangalizi ili kumsaidi motto Sesilia kupata
matumizi muhimu kama Dawa, kitanda kizuri kumsaidia Mgongo, Kiti maalum
cha kukalia na chakula chake ambachohutayarishwa tofauti na vyakula
tunavyokula.
Hoyce Temu
Mtayarishaji an Mtangzaji
Mimi na Tanzania
Email: hoyycet@gmail.com
Tovuti: www.miminatanzania.co.tz





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)