Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mbarali Modestus Kilufi siku alipokuwa akikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki.
Na, Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mbunge
wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi (51) (CCM)
aliyekamatwa mwishoni mwa wiki kwa kosa la kutishia kuzuru kwa kutumia
silaha amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu mfawidhi wa
wilaya ya Mbeya na kunyimwa dhamana.
Wakisoma
mashitaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Michael Mteite,
Mawakili watatu wa Serikali Griffini Mwakapeje, Basilius Namkambe na
Emma Msofe, wamesema kuwa Mbunge huyo alimtishia kumzuru Jordan Masweve
March 16 mwaka huu wilayani Mbarali.
Wamesema
kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria 89 cha mabadiliko ya
sheria ya mwaka 2002 kifungu kidogo cha 2(a) sura ya 16 ambapo
mshitakiwa alikana shitaka.
Kesi
hiyo yenye namba CC/158/2011 baada ya mshitakiwa kukana shitaka
linalomkabili, ndipo wakili wa Mbunge huyo Simon Mwakolo aliiomba
mahakama hiyo dhamana kwa mteja wake.
Baada
ya ombi hilo kusikilizwa na mahakama, Hakimu Mteite alikataaombi hilo
na kwamba mtuhumiwa atatakiwa kepelekwa mahabusu hadi Octoba 24 mwaka
huu wakati Mahakama ikiendelea kufikiria masharti ya dhamana.
Baada ya hapo kesi ikaahirishwa na Mbunge huyo kupelekwa mahabusu katika gereza la Ruanda lililopo mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)