MATUKIO ZAIDI YA KUUNGUA TRANSFOMA LILILO JIRANI NA TBC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MATUKIO ZAIDI YA KUUNGUA TRANSFOMA LILILO JIRANI NA TBC


Maaskari wakiwasili eneo la tukio kulinda usalama.
Moto ukishika kasi.
KITUO cha kurusha matangazo ya luninga kwa mfumo wa digital cha Star Times, kilichopo katika eneo la ofisi za Shirika la Utangazaji laTaifa (TBC1) zilizoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, mchana huu kiliwaka moto baada ya transoma mpya iliyofungwa kituoni hapo kulipuka na kuwaka moto. Juhudi za vikosi mbalimbali vya kuzima moto vilifika na kuuzima moto huo. Jumanne iliyopita transfoma ya awali ililipuka na kushika moto ambapo mpya iliyowekwa nayo ililipuka.

Mashuhuda wanasema chanzo cha moto huo ni transfoma hiyo mpya wakati ikifanyiwa majaribio ililipuka kutokana na mwingiliano wa jenereta kubwa la kampuni hiyo ambalo nalo lilishika moto.
Hakuna mtu aliyeumia katika tukio hilo isipokuwa mali kadhaa ambayo thamani yake haijajulikana iliteketea ikiwa pamoja na sehemu ya jengo moja lilikokuwa karibu na tukio ambapo lilishika moto.

Wakati moto ulipokuwa unashika kasi, wafanyakazi wa Star Times ambao ni Wachina walitaka kujitosa na kuingia ndani ya ofisi zao ili kuokoa mali zao, lakini polisi waliokuwa eneo hilo waliwazuia kwa hofu kwamba tenki la mafuta ya dizeli lililokuwa karibu na ofisi hizo lingeweza kulipuka na kuwasababishia madhara.

Vikosi vya zimamoto vikiwasili eneo la tukio.Jenereta kubwa lililokuwa likitumika na kituo hicho likiteketea kwa moto.
Wafanyakazi wa vikosi vya kuzima moto wakizima jenereta lililoshika moto.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia akilinda usalama.
Baadhi ya vitu vikiokolewa.
Mmoja wa maofisa wa polisi akitoa maelekezo kwa vijana wake.
Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya Kinondoni, Christopher Masasi, akielezea mazingira ya tukio hilo ingawa alisema bado chanzo hakijajulikana.

PICHA : RICHARD BUKOS  / GPL 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages