Mtuhumiwa Bwana
Mohamed Mwawipa ambaye alimshinikiza mkewe Nuru
Masuba kunywa sumu baada ya
kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu shilingi laki nne na elfu
hamsini akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe
Mwili wa marehemu
Nuru Masuba aliyeshinikizwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kumwibia
fedha shilingi laki nne na elfu hamsini na Mumewe Mohamed Mwawipa
akipelekwa kuhifadhiwa kaburini, baada ya uchunguzi wa daktari na
polisi kukamilika.
Mweyekiti
wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John
Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu
alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.
Na mwandishi wetu
Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50
mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani
Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za
kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi
laki nne na elfu hamsini.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza
kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na
mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya
mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.
Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa
kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda
tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke
huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu
kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate
Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema
kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi
pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya
Mbarali.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)