Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , akitoa
heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Mama Han Bing mke wa
Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
aliefariki siku kadhaa zilizopita jijini Dar es Salaam kwa kuuwawa na
majambazi wasiojulikana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,akiwa na viongozi mbali mbali kwenye ibada ya kumuombea Marehemu
Picha ya Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
Kamanda
wa kanda maaluum ya kipolisi ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akiwapa
pole wana jumuiya ya wachina waishio Tanzania jijini Dar es salaam
wakati walipokwenda kuaga mwili wa Mama Han Bing alieuwawa na majambazi.
Wanajumuiya
ya Kichina waishio nchini Tanzania wakiwa kwenye misa ya kumuombea
Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara
wa kichina nchini Tanzania
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole Mume wa Marehemu,Bw. Bing ambaye
alikuwa ni mwenye huzuni mkubwa sana wa kuondokewa na mke wake
aliyeuwawa na Majambazi siku kadhaa zilizopita.
Mama Salma Kikwete akimfariji Mtoto wa Marehemu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akitoa
salamu za pole wa wafiwa na wanajumuiya ya kichina katika msiba huo.
Mume wa Marehemu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na wanafamilia wengine kwenye misa ya kumuombea Marehemu.
Mmoja wa Kina Mama wa Kichina akilia kwa huzuni baada ya kuondokewa na ndugu yao.
Mmoja wa wanafamilia akimbembeleza mtoto wa Marehemu.
Picha na Mwanakombo Jumaa- Maelezo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)