| Prof. Nkoma wa TCRA akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais alipoingia ndani ya banda la Tanzania. |
| Bwana Victor Nkya Akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais |
| Bwana Masika wa TAYOA akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais |
Tanzania
inawakilishwa katika Mkutano na Maonesho haya na Waziri wa Mawasiliano
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Viongozi mbali kutoka wizara
hio, Mkurugenzi mkuu wa malmaka ya mawasiliano Tanzania, prof. John
Nkoma akiambatana na watumishi wa Mamlaka hio.
Aidha
Tanzania ina banda la Maonesho ambalo taasisi zifuatazo zinafanya
maonesho: Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, wanaoonesha
jinsi Mkongo wa Mawasiliano ulivyoIshaunganishwa na nchi zote jirani naTanzania,
Wizara ya Elimu na Maendeleo ya Ufundi, wakielezea mradi mashuhuri wa
Tanzania beyond Tomorrow, TAYOA, ambao wanaonesha matumizi ya teknolojia
kwa ajili ya vijana katika kupambana na ukimwi pamoja na umaskini,
TzNIC, ambao wanonesha matumizi na Maendeleo ya usimamizi warajisi ya .TZ kwa Watanzania badala ya matumizi ya .Com.
Makamu wa Rais, Dr. Gharib Bilal, akiongozana na Mama Zakia Bilal wametembelea Banda la Tanzania na Mabanda ya nchi za Afrika mashariki, Malawi, Ghana na Malawi.
Makamu wa Rais, Dr. Gharib Bilal, akiongozana na Mama Zakia Bilal wametembelea Banda la Tanzania na Mabanda ya nchi za Afrika mashariki, Malawi, Ghana na Malawi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)