Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, akipita
kukagua gwaride wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wizara hiyo,
yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo mchana.
Mbunifu
wa Mitindo Fatma Amour ,akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam. Fatma ni miongoni wa
Wajasiriamali waliobahatika kupewa udhamini na Umoja wa Mataifa
kushiriki katika wiki ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kuonyesha
bidhaa zao. (Picha na http://dewjiblog.com/
Wasanii wa Kikundi cha Tanzania House ofa Talent (THT) wakitoa burudani katika sherehe za maadhimisho hayo.
Wawakilishi
kutoka Balozi mbalimbali na viongozi wa Serikali wakifuatilia sherehe
hizo zilizokuwa zikendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Mabalozi
wastaafu nchini wakishangilia moja ya hotuba iliyosomwa katika
maadhimisho ya miaka 66 ya Umoja wa Mataifa na maadhimisho ya miaka 50
ya Uhuru wa Tanzania iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Maadhimisho
hayo yalienda pamoja na wiki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa kwa kuonyesha shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Wizara
hiyo.
Wanafunzi
wa shule ya Jitegemee kwa upande wa kwaya wakitoa burudani katika
kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na miaka 66 ya Umoja wa
Mataifa.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)