IGP Said Mwema:Natanganza Dau La Shilingi Milioni 5 Kwa Mtu Yeyote Atakaefanikisha Kupatikana Kwa Mtu aliyemjeruhi Mtoto Adam Robert {Albino}Huko Geita - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

IGP Said Mwema:Natanganza Dau La Shilingi Milioni 5 Kwa Mtu Yeyote Atakaefanikisha Kupatikana Kwa Mtu aliyemjeruhi Mtoto Adam Robert {Albino}Huko Geita


Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na  kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages