Na Mwandishi Wetu
BAADA
ya Bonanza la kwanza la wadau wa burudani ambao ni kampuni ya Media
Entertainment Group kwa kushirikiana na bendi ya Extra Bongo kufana,
hatimaye wadau hao wameamua kunogesha ubora wa Bonanza la leo ambalo litakuwa la aina yake.
Mwenyekiti
wa Bonanza hilo linalofanyika kila Jumapili kwenye uwanja wa TP, Sinza
Uzuri jijini Dar es Salaam, Rachel Mwiligwa alisema jana jijini Dar es
Salaam kwamba tofauti na wiki iliyopita, bonanza la leo limeongezewa
burudani kibao, ambapo mbali na kuongezeka kwa timu shiriki, pia
kutakuwepo na burudani ya ziada kutoka kwa bendi mbili, za Extra Bongo
inayoongozwa na Ally Choki na Bantu Group chini ya Commandoo Hamza
Kalala.
Mwiligwa
alisema kutokana na kuongezeka kwa timu, wameamua kuweka zawadi ya jezi
kwa ajili ya kushindaniwa, ambazo zimetolewa na mdau maarufu
anayemiliki maduka ya jezi, Spear Mbwembwe.
Alisema
bonanza la leo litakuwa funga kazi kwani pamoja na mechi za ushindani
mkali kutoka kwa timu mbalimbali zitakazoshiriki, Extra Bongo na Bantu
wameahidi kupagawisha mashabiki mara mbili ya walivyofanya wiki
iliyopita.
Mmoja
wa viongozi wa bendi hiyo Ramadhani Masanja Banzastone aliwaambia
waandishi wa habari jana kwamba wameahidi kutoa burudani ya ziada ambapo
yeye, Ally Choki na Roggart Hegga Katapilla, watapiga nyimbo zao zote
walizotunga wakiwa katika bendi mbalimbali.
Kuhusu
timu, Mwenyekiti Mwiligwa alisema timu nyingi zimethibitisha kushiriki,
ingawa aliwataka washiriki kuwahi kufika kwani Bonanza litaanza kuanzia
saa 2:00 asubuhi. Aidha aliwashukuru baadhi ya wadau ambao wamekuwa
wakisaidia ufanikishwaji wa Bonanza hilo zikiwemo timu za Wahenga, MSD,
Villa, Shein, Uongozi wa baa ya Freetown, Goodluck wa baa ya Meeda,
Masoud Wanani, Mzee wa Pamba, Fred Mopao, Nassoro Fundikira na wengineo
kibao.
Aidha
kutakuwepo na ugeni wa wanamuziki wanaounda kundi la Mapacha Watatu,
Kalala Junior, Khalid Chokoraa na Jose Mara ambao watabadilishana mawazo
na wadau.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)