Dr Julie Makani akitoa machache
Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London
Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake
Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani
Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo
Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo jumanne tarehe 18 octoba
2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr Makani amepokea tuzo
hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD)
ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha
Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake
kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo
na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa
damu)
Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya
Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya
Anaemia kwenye ugonjwa Sickle Cell
Ni matumaini yake kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na
matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima
wa afya na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Watanzania wote Urban Pulse tunapenda kumpongeza DR Makani kwa mafanikio hayo. | ||





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)