Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Jane Dogani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma Kwa Wateja wa benki hiyo jiijini Dar ers Salaam jana. Kushoto
ni Allan Maro na Mark Peter maofisa wa NBC katika kitengo cha Huduma kwa Wateja.
ni Allan Maro na Mark Peter maofisa wa NBC katika kitengo cha Huduma kwa Wateja.
NATIONAL BANK OF COMMERCE

TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI YA NBC YAZINDUA WIKI YA
HUDUMA KWA WATEJA
Dar es Salaam Oktoba 17, 2011
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua Wiki ya
Huduma kwa Wateja inayoanza leo hadi tarehe 22 Oktoba mwaka huu. NBC inaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
inayoanza leo katika matawi yote ya
benki hiyo nchini ikiwa na kauli mbiu ya ‘Mteja Kwanza’
Akizungumza Meneja wa Kitengo cha Huduma Bora kwa
Wateja wa Benki ya NBC, Mama Jane Dogani anasema kauli mbiu ya Wiki ya Huduma
kwa Wateja ya NBC inayosema ‘Mteja
Kwanza’ ni dhihirisho la jinsi gani mteja wa benki hiyo alivyo muhimu na kuwa
mhimili mkuu wa maendeleo ya Benki ya NBC.
“Madhumuni makubwa katika wiki hii ni kutaka kuwa
karibu zaidi na wateja wetu ili tuweze kubadilishana mawazo tupokee maoni yao kuhusu ni nini
wangependa tuwafanyie au ni wapi na kipi wangependa tukibadilishe ama
kukiongeza,” anasema Mama Dogani.
Katika Wiki hii ya Huduma kwa Wateja wa NBC wateja
wanaweza kufika katika matawi ya benki hiyo, kuuliza maswali kuhusu huduma na
bidhaa mbalimbali zinazotolewa na NBC. “Wataalamu wetu wamejipanga vizuri katika matawi
yote ya benki yetu hivyo wateja msisite kufika katika matawi hayo ambako mtapata
majibu sahihi kuhusu huduma zetu, aina mbalimbali ya akaunti tunazotoa, bidhaa
na huduma mpya, masuala ya mikopo na mambo yoyote ya kibenki yanayoihusu NBC,”
anasema.
Katika Wiki ya Huduma kwa Wateja NBC mbali na
kuandaa mikutano na wateja wake watakaofika katika matawi hayo pia
imeandaa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya
wateja wake ikiwa kama ishara ya shukurani kwa wateja wake na pia kufurahia
mafanikio ya benki yao
iliyo karibu kila mahali yaani Benki ya NBC.
“Itakuwa wiki yenye mambo mengi ya kuvutia kutoka
NBC, natoa wito kwa wateja wetu wasikose kutembelea matawi yetu kujionea
wenyewe jinsi benki yao ilivyojipanga kuwahudumia.Wale ambao hawajafungua
akaunti nasi basi huu ndio wakati muafaka wa kufika katika matawi yetu kufungua
akaunti na kupata huduma za kibenki kutoka kwa wahudumu wetu wapole na
wakarimu,” anasema Mama Dogani.
Benki
ya NBC iliundwa Aprili 1, 2000 baada ya ubinafsishwaji na kuuzwa kwa Benki ya
ABSA ya Afrika Kusini inayomiliki Hisa asilimia 55 huku Serikali ya Tanzania ikibaki na Hisa za
asilimia 30 na zinazobaki asilimia 15 zikimilikiwa na Mashirika ya Kimataifa ya
Kifedha. Benki ya NBC ina mtandao wa
matawi 53 nchini kote na mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 250.
MWISHO.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)