Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor
Mtandao wa mawasiliano waendelea kutoa gharama nafuu za mawasiliano kwa nchi za afrika mashariki Sasa kuongea na jirani zetu afrika mashariki kwa punguzo la hadi sh 2 na senti 50 tu kwa sekunde. Gharama nafuu ya mawasiliano ni nyezo muhimu katika kusaidia kukuza uchumi wa nchi
Dar es Salaam, Tanzania 02 Octoba 2011 Airtel
Tanzania imetangaza gharama mpya za kupiga simu Kenya na Uganda.
Kupitia punguzo hilo wateja wa Airtel ndugu na jamaa zao sasa wataweza kufanya biashara kwa urahisi hasa zile zinazohusisha kuvuka mipaka ya nchi yetu na kuhusisha nchi za Kenya au Uganda kwa punguzo nafuu sana la Tsh 2 na senti 50 tu badala y sh 5 na senti 16
“Huu
ni muendelezo wa kati ya dhamira endelevu tulizonazo Airtel kuwapa
unafuu hasa wafanya biashara kuweza kufanikisha mahusiano yao kibiashara
kati ya nchi moja hadi nyingine”
Akisisitizia
Dhamira hiyo ya kupunguza mawasiliano simu za kwenda nje ya nchi
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor aliendelea kusema “Airtel
ni mtandao pekee unaotoa mawasiliano yenye uhakika zaidi kwa nchi za
afrika mashariki. Airtel bado tutaendelea kuongoza kwa kutoa mawasiliano
bora na kwa gharama nafuu zaidi tukiwa tunalengo thabiti la kuondoa kabisa changamoto ya mawasiliano katika nchi za Afika Mashariki”
Maendeleo
ya uchumi wa jamii huwezeshwa na muunganiko wa jitihada au nyenzo
nyingi, hivyo ninaimani kuwa kuvuka kwetu mpaka na kurahisisha
mawasiliano ni dhairi itasaidia kukuza na kuboresha maisha ya jamii
zote. Hili imewezeshwa zaidi na wateja wanaendelea kujiunga kila siku
pamoja na dhamira yetu ya kutendelea kusambaa nchi za jirani” aliongeza
kusema, Sam





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)