Adolf Hitler; Ukweli Uliofichika…..(1) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Adolf Hitler; Ukweli Uliofichika…..(1)

https://mail.google.com/mail/?ui=2&ik=3530edf2ab&view=att&th=132be469c2c69b28&attid=0.1&disp=inline&realattid=file0&zw 
Na Nova Kambota Mwanaharakati,
Nimekuwa nikifanya utafiti kuhusu maisha ya Adolf Hitler kupitia maandiko mbalimbali  na niseme wazi katika dunia ya leo  “mwendawazimu mkubwa”  ni mtu anayepingana na fikra za kimagharibi ndiyo kwa wasomi wetu wa sasa wenye mtazamo wa kizungu ni vigumu kuyaona mambo katika uhalisia wake bali katika mtazamo wa kiulayaulaya na Marekani. Maandiko na mtiririko wa mantiki unabainisha kuwa fikra za anayeitwa dikteta Adolf Hitler zingalipo mpaka leo hii tena zinaongoza sio tu Ujerumani bali Ulaya na Marekani, pengine kuna watu watapinga hili , ila sina hofu, najua kwanini watanipinga? “hawasomi” na “hawapendi kusoma” na zaidi wamefumbwa wasione vinavyoonekana, naam! Naandika kuibua mjadala, naandika kunyoosha palipopinda, naandika ili tujifunze  kufikiri.
 
Kama unadhani fikra za Adolf Hitler zimekufa au wazungu hawapendi mawazo yake nasema basi hesabu “Maumivu” narudia tena hesabu maumivu, kabla hujaendelea kubisha hebu tafuta kitabu cha Adolf Hitler
kinachokwenda kwa jina la “Mein Krampf” kilichopigwa chapa mnamo mwaka 1925. Mwenyewe Adolf Hitler alikiandika kitabu hiko akiwa gerezani mnamo mwaka 1923, inaelezwa kuwa kitabu hiko ndiyo ulikuwa mwongozo wa utawala wake baadae kuanzia mwaka 1933 mpaka 1945. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945 pengine kwa kukusudia au kwa hulka yao ya kuficha ukweli wazungu na wamarekani
wamefanikiwa kuficha ukweli kwa zaidi ya miongo mitano kuwa “fikra za Adolf Hitler ndiyo mwongozo wa mataifa hayo ya kibeberu” na vyovyote itakavyokuwa ukweli utabaki hivyo kuwa Mein Krampf(My Struggle) au kwa Kiswahili kinaitwa “Mapambano Yangu” ndiyo mwongozo wa Ulaya na Marekani kwa maana nyingine tunaweza kunyumbulisha mantiki kwa kuhitimisha kuwa “Mawazo ya Hitler yanaitesa Afrika mpaka leo”.
 
Ukipitia kitabu hiko utakutana na kauli hii “Those who want to live, let them fight, and those who do not want to fight in this world of eternal struggle do not deserve to live.Adolf Hitler Mein Kampf”  kwa tafsiri nyepesi ya Kiswahili Adolf Hitler hapa anamaanisha wanaohitaji kuishi hawana budi kupambana, na wale
wasiotaka kupambana basi hawastahili kuishi Dunia hapa.  Naam! Haya ndiyo mawazo ya kiongozi wa Manazi Adolf Hitler , sasa je hebu tuone undani wa kauli hii na je nani anaitekeleza kwa vitendo? Na kwa mapana yapi?

Mpaka leo hii hakuna ubishi Ulaya na Marekani wako katika mapambano ya kufa na kupona kuhakikisha ubeberu wao unazidi kuimarika na zaidi ya yote mirija yao ya kunyonyea inazidi kufyonza maliasili za Afrika . Mapambano ya wazungu ni kuhakikisha kuwa Afrika inaendelea kuwa masikini, haya ndiyo mawazo ya Adolf Hitler ambayo yanakumbatiwa na mabeberu wa Ulaya na Marekani, wasiyapende vipi wakati yanawasaidia?
Sasa kwanini wadanganye dunia kuwa hawampendi Hitler? Waswahili wanasema “ukipenda boga sharti upende na ua lake”, Je iwapo ni kweli Hitler ni mbaya kwanini wakumbatie na kuzisujudu fikra zake?  Kuna
nini hapa?
 
Naam! Hii ndiyo kwanza sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii ya kusisimua , jiandae kusoma sehemu ya pili itakayoeleza kwa undani uhusiano kati ya mawazo ya Adolf Hitler na ubabe wa mataifa ya Ulaya na Marekani. Asante kwa kusoma!

Tanzania, East Africa
Saturday, October1, 2011.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages