WIZARA YA UCHUKUZI YASAINI MKATABA NA KAMPUNI YA SINOHYDRO CORPORATION LTD KUKARABATI VIWANJA VYA NDEGE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WIZARA YA UCHUKUZI YASAINI MKATABA NA KAMPUNI YA SINOHYDRO CORPORATION LTD KUKARABATI VIWANJA VYA NDEGE

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Suleiman Suleiman (kushoto) na Mhandisi Mwandamizi wa Kampuni ya  SINOHYDRO CORPORATION LTD, Tawi la Afika Mashariki, Qin Chao, wakitiliana saini mikataba ya ukarabati wa kiwanja  cha ndege  cha Kigoma, wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini iliyofanyika jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania katika sekta ya Uchukuzi, Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TAA) Suleiman  Suleiman akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kusaini mikataba ya ukarabati wa viwanja vya ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhiisho ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika sekta ya Uchukuzi.
 Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Uchukuzi waliohudhulia hafla hiyo leo.
Picha ya pamoja baada ya hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages