Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami Azindua Bodi Ya Vipimo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami Azindua Bodi Ya Vipimo


Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami (kulia), akiagana na Mjumbe mpya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Paskali Massawe  baada ya kuzindua bodi hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Massawe ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Paskali Massawe ambaye ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Vipimo (WMA), akijitambulisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam. Mwenyekiti aliyemaliza muda wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Hosea Kiula ambaye pia kateuliwa kuwa mjumbe wa bodi hiyo. 
Waziri Chami (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake, Hosea Kiula. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Bodi, Rose Lugembe.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Hosea Kiula (kulia), akiagana na Mjumbe mpya wa bodi hiyo, Paskali Massawe baada ya hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo kumalizika, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa.Massawe ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Baadhi ya wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Vipimo (WMA), wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Viawand, Biashara na Masoko, Cyril Chami (wa tatu kulia), baada ya kuzinduliwa mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mjumbe, Paskali Massawe ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa EWURA, Mwenyekiti wa zamanni wa bodi hiyo ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe, Hosea Kiula, Mwenyekiti mpya wa Bodi, Rose Lupembe na kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joyce Mapunjo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages