Mbunge wa Sumve (CCM,)Mheshimiwa Richard Ndasa,akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari,(hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam, kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Mwanahalisi toleo
la wiki hii ambazo zilielezea hatua ya bunge kutaka kupiga kura ya
kutokuwa na imani na Rais, kufuatia sakata la kusimamishwa kazi kwa
aliyekuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na
kurudishwa tena kazini. Kulia ni mbunge wa Ilala Mussa
Azzan Zungu.Habari na Picha na Mdau Victor Makinda
--
Akizungumzia habari iliyochapishwa na gazeti hilo,Mheshiniwa
Ndasa alisema kuwa gazeti la Mwanahalisi limechapisha habari za
kizushi na za uongo zenye lengo la kufitinisha Bunge na
Rais.Aliongeza kusema kuwa wakati Jairo anarudishwa kazini na Katibu
Mkuu, Luhanjo, Bungeni mjini Dododma hapakuwa na hatua yoyote ya
wabunge kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kufuatia
kuruhusiwa kwa Jairo kuendelea na kazi.
Akifafanua kuhusu
uamuzi wao wa kutolea ufafanuzi na kukanusa habari hiyo, Ndasa alisema
wao kama wabunge wa CCM, hawatopenda kuona kiongozi wa nchi
anazushiwa habari zisizo na ukweli wowote.
Akijibu swali kwa nini
wao kama wabunge wajitokeze kukanusha taarifa hiyo ikiwa Ikulu ina
kurugenzi ya Mawasiliano, Bunge linaongozwa na Spika, Pia yupo Waziri
mkuu, ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ambao
kimsingi moja kati ya mamlaka hizo ndizo zilizotakiwa kufafanua au
kukanusha habari hiyo, Ndasa alisema, wao hawajatumwa na Ikulu wala
mamalaka yoyote bali wametumwa na dhamira yao kama Watanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)