Bi Gloria Mongello,Meneja Mradi wa
TWENDE, ,Pembeni ni Bi Husna Rousse wa Zero 2 Twelve , katika
mkuatano na waandishi wa Habari katika ofisi ya Mustafa Hassanali
Dar-es-salaam.
Gloria Mongella,Meneja Mradi wa Twende akiwa
na Juma Mbaruku kutoka Ultimate Security,na Bi Husna Roussos wa ZERO 2
Twelve , katika mkuatano na waandishin wa Habari tarehe
13-sep-2011,Dar-es-Salaam
---
Kwa mwaka wa pili TWENDE,
itafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Hafla hii ya jumuia
itakayokua ikifunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00
jioni kwa siku tatu mfululizo 15-17 Septemba 2011
Kiingilio TWENDE ni bure kwa watu wote, ili
kuweza kusababisha jamii ijihusishe kikamilifu na wanawake
wajasiriamali na ndivyo hivyo kwa wanawake wajasiriamali kupata nafasi
ya kuonyesha bidhaa na huduma zao ili kuweza kuwa na mawasiliano na
kuendelea katika biashara Tanzania.
Meneja Mradi wa TWENDE,”Gloria Mongella alisema,Tunategemea
maudhurio makubwa kwa wanawake zaidi mwaka huu, kwakua kiingilio ni bure
na pia kwa sababu viwanja vya Mnazi Mmoja vipo katikati ya mji na
kusababisha iwe rahisi kwa watu wengi kuudhuria” .
TWENDE itafunguliwa rasmi Alhamisi ya tarehe 15 Septemba 2011
Saa 5:00 asubuhi, na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto
,Muheshimiwa Sophia Simba.
Bi Mongella aliongeza “Tunajisikia faraja kubwa kwa hafla hii
ya TWENDE kufunguliwa na Waziri ,kwahivyo tunawahamasisha wanawake wote
kuweza kuudhuria kwa wingi katika ufunguzi wa maonyesho ya TWENDE, na
kutumia nafasi hii katika kukutana na wanawake mbali mbali
wajasiriamali”.
TWENDE itakua na semina ya siku tatu ikidhamiria kuhamasisha
,kuelimisha na kuendeleza wanawake katika sekta mbalimbali
ikiwemo,afya,sheria,biashara,na risala za kuhamasisha
“Elimu ni uti wa mgongo katika jamii yetu, kwahivyo
tunawaamasisha watu wafike kwa wingi katika semina za TWENDE,ili waweze
kupata ufahamu kutoka kwa watu mbali mbali waliobobea
katika sekta ya biashara kama njia ya kujifunza mbinu
katika biashara na kufanya wanawake wawe bora katika ujasiriamali
Tanzania” alisema Hamis k.Omary,Meneja Masoko wa TWENDE.
Dhamira ya TWENDE,ni kutangaza nafasi ya mwanamke katika
maendeleo kitaifa kwa kutambua umuhimu na mafanikio ya
wanawake wajasiriamali wakiwemo na wale walemavu katika
kuwatengenezea ajira, kuwatambulisha wanawake
wajasiriamali kama mifano ya kuigwa,kusambaza taarifa za wanaofanya
vizuri katika biashara,kuwa na muungano wa wanawake
wafanyabiashara (TWENDE SACCOS), na kuwasaidia katika afya zao
,kujitegemea wenyewe, na kujitegemea kiuchumi.
TWENDE imedhaminiwa na Ubarozi wa Marekani wa Tanzania , Daily
News, Habari Leo, Delfina, Perfect Machinery, Ultimate Security, Global
outdoor systems, Dar life, Clouds FM, Vayle springs, Eventlites,
Coca-Cola na 361 Degrees.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)