Msaada wa pesa kwa Mtoto Sesilia Edward - Kupata Upasuaji India - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Msaada wa pesa kwa Mtoto Sesilia Edward - Kupata Upasuaji India

Hoyce Temu akiwa na mtoto Sesilia na wazazi wake nyumbani kwao wakati alipowatembelea.
Hapa akimkabidhi msaada wa fedha. 
 
Ndugu Watanzania,

Jumapili tarehe 11 Septemba, kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Chanel Ten, kilifanya Mahojiano na Mtoto Sesilia Edward mwenye matatizo ya moyo na anahitaji upasuaji wa haraka kuokoa maisha yake. Upasuaji huo unatakiwa kufanyika nchini India.

Jumla ya dola 15 sawa na shilingi milioni 24 za kitanzania zinahitajika kuokoa maisha yake. Kama asipofanyiwa upasuaji wa haraka la sivyo atapoteza maisha ndani ya Mwezi Mmoja.

Watanzania wameanza kuchanga kumsaidia motto huyu apate matibabu. Kupitia katika simu za mlezi wake anaeishi naye huko Mbagala Bwana Nyarugembe Peter Kambaliko katika nambari zifuatazo:
Tigo Pesa:- 0715 095797
MPESA: – 0762 962467
NMB Account: 2072517079
 
Hadi sasa zaidi ya shilingi milioni mbili zimekwisha changwa na bado Watanzania wanaendelea. Chonde chonde Watanzania, hata mia tano ni mchango. 

Usiache kutizama marudio ya kipindi Jumamosi saa 12:30 jioni, Chanel Ten ambapo mtasomewa kiasi cha fedha zilizokusanywa. Account ya NMB imefunguliwa kwa ajili ya hitaji hilo na namba za simu pia. 

Mtoto huyu ni Mzaliwa wa Kisarawe, yatima na anishi na mlezi aliemkuta akiwa taabani nyumbani kwao Segerea. Angetakiwa kufanya mitihani ya Darasa la Saba na wenzie mwaka huu lakini hali yake Haimruhusu. Angependa kuwa mwalimu. Mlezi wake Peter Nyarugembe, amejaribu kwenda kila mahali bila mafanikio ikiwamo Wizarani – Afya na hata hospitali ya Regency bila mafanikio.

OMBI KWA MAKAMPUNI YA SIMU:

Tunaomba wafungue account hizo ziweze kupokea fedha nyingi kwani kuna Account ya MPESA ilifungiwa.

Kwa makampuni yenye ufadhili mkubwa tafadhali piga simu 0767 – 262625 kupata maelezo zaidi toka kwa Hoyce Temu alierusha kipindi.

Asanteni Sana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages