Mwandishi wetu
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amewaagiza polisi kumhoji
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, kuhusu hatua yake ya
kupanda jukwaani na bastola kiunoni. Taarifa iliyopatikana na
kuthibitishwa na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambao hawakupenda
kutajwa, ilisema polisi wameagizwa kuwa baada ya kumhoji mbunge huyo,
wawasilishe ripoti hiyo kwake haraka iwezekanavyo.
Miongoni mwa mambo ambayo polisi
wameelekezwa kumhoji Rage ni pamoja na endapo anaimiliki bastola hiyo
kihalali. Mambo mengine ni sababu alizoeleza wakati anaiomba bastola
hiyo na hatua yake ya kwenda nayo kwenye mkutano wa hadhara.
“Tunasubiri
taarifa, tumewaagiza polisi wamhoji. Tunataka kujua mambo matatu; kama
silaha hiyo anaimiliki kihalali, pili madhumuni aliyoiombea na tatu
kwenda nayo kwenye public meeting (mkutano wa hadhara) wakati kuna
watoto, wanawake na watu wa aina mbalimbali,” kilisema chanzo chetu cha
habari kikimnukuu Nahodha na kuongeza: “Haiwezekani kwenda na silaha
tena nje nje kwenye mkutano kama ule. Sasa tunasubiri taarifa ya
polisi.”
Chanzo: Majira
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)