|
Wawakilishi wa
vijana wa Tanzania katika Bunge la Vijana wakipozi kwa picha katika
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza baada ya kuwasili nchini
humo kwa ajili ya kuwakilisha vijana katika Bunge hilo. |
Ubalozi
wa Tanzania Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde
kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament (
Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London.
|
Wawakilishi hao wakiwa
katika mahojiano. |
Mkutano
huo Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la
Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa
Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza
kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.
|
Pozi la picha
Ubalozini hapo.
Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha
vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge
hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano
wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"
Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda
kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na
pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.
|
|
Mahojiano
yanaendelea. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)