Mganga wa Kienyeji Maarufu kama Dr Manyaunyau.
Vijana hawa wakiwa Bara barani
wakimzungusha huyu Mnyama aina ya Paka, kwa akili zao wakiamini
wamemshika mchawi na wameamua kumsulubisha. Vitendo hivi vya kikatili kwa wanyama
vimekuwa vikiendelea mara kwa mara hasa katika maeneo ambayo yana
mrundikano wa makazi ya watu, na hata vingine vikionyeshwa kwenye
luninga zetu lakini wahusika wa haki za wanyama wakivitazama tu
vikiendelea bila kuvikemea wala kuwachukulia hatua wale wote
wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.
Kwa mataifa ya wenzetu ni lazima upate hukumu ya kifungo kwa kufanya vitendo hivi. KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika waweze kutimiza majukumu yao na ikiwezekana wawachukulie hatua hawa wote wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)