Mtoto Cecilia Edward ambaye
anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo
amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia
kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu
anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.
Cecilia
amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New
Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka
huu.
Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko
inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo
kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya
faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia
ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa,
tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo
lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya
kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
Mtoto huyu aliondoka hapa nchini
jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana
na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja na mlezi mmoja
mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa na madaktari tayari kwa
uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
Kipindi
cha Mimi na Tanzania kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na
makampuni mbalimbali yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya
matibabu. Shukrani za pekee ziifikie hospitali ya regency hasa daktari
Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao
wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa Sesilia, mzazi na daktari
ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi sasa.
Watanzania,
pamoja tumeweza tena. Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja
wanaosumbuliwa na tatizo hili, hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa
bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu kwa maombi ili upasuaji
anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi yake Mungu mtoto
huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto wengine.
Mungu mbariki Sesilia.Amen!
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)