Ofisa
Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude (Kulia) akiwakabidhi Tshirt
wawakilishi wa Tanzania kutoka timu ya taifa ya Mbio za Mashua
watakaoshiriki mbio za "All African Games Sailing" zitakazofanyika
Maputo Msumbiji kuanzia Septemba 3 hadi 11. Vodacom imeidhamini timu
hiyo kwa shilingi milioni 8/-.
Wawakilishi
wa Tanzania kwenye mashindano ya mbio za mashua za "All African Games
Sailing" zitakazofanyika Maputo Msumbiji kuanzia Septemba 3 hadi 11
wakiwa wameshikilia bendera ya Taifa waliokabidhiwa kabla ya kuondoka.
Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na habari za Mtandao wa Vodacom
Tanzania Matina Nkurlu,Ibrahim Kaude Ofisa Udhamini wa kampuni hiyo
iliyodhamini timu hiyo kwa shilingi Milioni 8/-.
Wawakilishi
wa Tanzania kwenye mashindano ya mbio za mashua za " All African Games
Sailing" zitakazofanyika Maputo Msumbiji kuanzia Septemba 3 hadi 11
wakiteta jambo mara baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa. Vodacom
Tanzania imeidhamini timu hiyo kwa shilingi milioni 8/-.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imewadhamini washiriki watatu
wa Timu ya Taifa ya Mbio za Mashua kwenda Maputo Msumbuji kuliwakilisha
taifa kwenye mbio za mashua zitakazofanyika Septemba 3 hadi 11 kwa
shilingi Milioni 8/-.
Wachezaji
walioenda kuliwakilisha taifa kwenye mbio hizo zitakazoshirikisha
baadhi ya nchi za Afrika 'All African Games Sailing' kutoka timu hiyo
inayofanyia mazoezi yake kwenye ufukwe wa Yacht Club ni Watanzania
Mwambao Helef, Halife Mpondi na Hassan Said wameondoka leo (jana)
kuelekea nchini Msumbuji.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mashua Tanzania (TSA) Phillemon
Nassari amesema kuwa ana uhakika vijana wake ambao wamefanya mazoezi
makali kwa kipindi cha miezi mitatu wataliwakilisha vema taifa na
kuliletea medali ya dhahabu.
Akifafanua
Nassari alisema kuwa mbio hizo zitakazoshirikisha mataifa mbalimbali ya
Afrika zitakuwa na changamoto baada ya kila nchi kudai kwamba
imejiandaa vizuri ili kuwa bingwa wa jumla kwa mashindano hayo.
"Fedha
hizi zilizotolewa na Vodacom Tanzania ni matumaini yetu zimetoa hamasa
kwa washiriki wetu kwenda kufanya vizuri msumbiji. Wamejiandaa vya
kutosha kwa takribani miezi nane ambapo kila wiki walikuwa wakifanya
mazoezi mara moja kwenye ufukwe wa Yatch Club," alisema Nassari.
Mbali
na hayo Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Utendaji wa TSA aliiomba serikali
kuigeukia na kuitilia uzito michezo mingine ikiwemo ya baharini hususan
wa mashua.
Nae
Alli Bush ambaye ni bingwa wa mashua kwa Afrika aliekuwa akifanya
mazoezi na wawakilishi hao alisema amewakubali na kwamba vijana hao
wameiva kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
Kwa
upande wake Ibrahim Kaude ambaye ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania
amesema kwa kuwa kampuni yake imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali
nchini imeona pia ni vema kuwekeza katika mchezo huo wa mashua nchini.
"Tunajisikia
fahari kuwa mmoja ya wadau waliofanikisha kusafiri kwa timu hiyo ya
Taifa ya mbio za mashua kwenda mjini Maputo na tunaendelea kudhamini pia
michezo mingine lengo likiwa kupandisha hadhi ya Tanzania katika tasnia
ya michezo duniani," alisema Kaude.
Mwakani
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji mashindano hayo ya mbio za mashua za
All African Games Sailing yatakayofanyika Agosti 4 hadi 14 kwenye
ufukwe wa Msasani chini ya usimamizi wa Yatch Club.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)