Baadhi ya Washiriki wa Mbio za Mashua,
zijulikanazo kama TANZACAT wakipunga Mikono kuashirika kuanza kwa
mbio hizo zilizozinduliwa rasmi jana katika Klabu ya Yatch jijini na
kudhaminiwa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Baadhi ya Washiriki wa Mbio za Mashua,
Zijulikanazo kama TANZACAT wakianza Mbio hizo jana katika Ufukwe wa
bahari ya Hindi eneo la Klabu ya Yatch jijini Dar es Salaam ambapo
Mashindano hayo yanayochukua siku saba yanadhaminiwa na kampuni ya Simu
za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus
Zervos akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo
zilizoshirikisha mataifa 16 na kuwashukuru wadhamini wakuu Kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mshiriki wa Mbio za Mashua zijulikanazo
kama TANZACAT, Belia Klaassen, aliyewahi kushiriki mbio hizo kwa miaka
kumi nchini Tanzania akielezea namna anavyofurahia kushiriki mashindano
hayo tena na jinsi yalivyoboreshwa zaidi jana jijini Dar es salaam
Mmoja wa washiriki wa mbio za mashua
zijulikanazo kama TANZANCAT Evelyne Geubbels (kulia) akieleza namna mbio
hizo za ufunguzi zinazodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom Tanzania zilivyofana katika Klabu ya Yatch jijini, kushoto ni
mshiriki mwenzake Jerome Vant Pad Bosch.
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus
Zervos (wa pili kulia)akiwa na baadhi ya washiriki wa mbio hizo mara
baada ya ufunguzi wa mbio hizo jana jijini ambapo zitaendelea kwa muda
wa siku saba na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)