Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Jordan Rugimbana (kulia)akisalimiana na moja ya wanafunzi wa
shule ya Msingi Mgulani ambapo alifika shuleni hapo kupokea msaada wa
madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kutoka
Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya
Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni
Mgulani,Tandika,Kizuiani,Muongozo na Kilamba. Hafla hiyo imefanyika
katika shule ya msingi Mgulani jijini Dares Salaam.Kushoto ni Mkuu wa
kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akiwasalimu baadhi ya wanafunzi wa
shule ya Msingi Mgulan.
wanafunzi wa shule ya Msingi Mgulani wakifurahia na
kucheza Kiduku baada ya hafla hiyo ya makabidhiano, Jamani kiduku
nomaaaaaaaaa!!!!
*******************************************
Ni awamu ya pili kampeni ya madawati 1000. Lengo
kupunguza uhaba wa madawati s/msingi
Ikiendelza utamaduni wake wa kusaidia jamii kwa lengo la kubadili maisha mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo umekabidhi madawati mia mbili na hamsini ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni ya utoaji wa madawati katika shule za msingi katika mkoa wa Dar es salaam yanayofikia madawati mia tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni arobaini na tano.
Akikabidhi madawati hayo leo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambae anakaimu pia Ukuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule amesema kampuni yake inatambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama amana muhimu ya kuwajengea mazingira ya maisha bora ya kujitegemea na pia kulisadia taifa.
"Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo da ndio maana Vodacom kampuni inayoungwa mkono na watanzania zaidi ya milioni kumi ikaamua kuonesha upendo kwa kuwa na kampeni kamambe ya kusaidia madawati mashuleni"Amesema Mkuu wa Vodacom Foundation.

Jumla ya madawati 1000 yenye thamani ya shilingi 89,000,000/= yatakuwa
yametolewa na Vodacom kwa shule za msingi kati ya April na Oktoba mwaka
huu.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)